Top Leaderboard Advert

ZSSF

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

PBZ_new_logo

Zanzibar Diaspora

Interactive

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Tuesday, August 23, 2016

'UKUTA' WAPIGWA MARUFUKU JIJINI DAR


KUTOKA MAGAZETI YA TANZANIA YA LEO TAREHE 21 AUGUST, 2016!

Polisi: Tumeanza kuvunja UKUTA,Lowassa: Tumejiandaa, CP Hamdani: Mazoezi hayahusiani na UKUTA, UVCCM kuandamana nchi nzima Agosti 31. Pata dondoo za uchambuzi wa magazeti hapa.

Muonekano wa moja ya ndege mpya za Air Tanzania

Huu ndio muonekano wa moja ya ndege mpya za ATCL zinazotarajiwa kutuwa nchini Tanzania mwezi ujao.
Ndege hizi zipo katika hatua za mwisho za kuwekwa rangi na nembo za Shirika la ndege la ATCL ambayo ni Twiga anayekimbia...

Kwa sasa ATCL imetangaza nafasi za marubani,Wahandisi na Cabin Crew wapya kwa ajili ya kuanza upya Operation ndani ya nchi na baadae nje ya nchi.Nafasi zilizotangazwa ni Dash8-Q800 Mechanical and Avionics Certifying Engineers nafasi 6,Co-Pilot Dash8 nafasi mbili,Pilot in Command Dash8 nafasi 2, na Cabin Crews nafasi 18.

Kwa marubani ni mkataba wa miaka mitano kazini,Wahandisi mkataba wa mwaka mmoja na wakati Cabin Crews ni miaka mitatu tu.Karibu Sana Air Tanzania 
  

https://www.jamiiforums.com/threads/muonekano-wa-moja-ya-ndege-mpya-za-air-tanzania.1101114/

Mgomo wa kisiasa ulivyomrejesha kwenye umaskini mjasiri amali mwanamke kisiwani Pemba

  • Kwa siku akivuna shilingi 150,000 sasa hazidi shilingi 5000
Na Haji Nassor, Pemba

“MIMI na umaskini tulishaachana kitambo, lakini sasa naurejea taratibu maana…!!!!...’’,aliniambia mwanamke huyo huku akipata kigugumizi.

Ni mcheshi na mchangamfu wakati wote na hasa anapokuwa kwenye biashara yake ya duka la vinywaji na vyombo vya matumizi ya nyumbani eneo la Wawi wilaya ya Chakechake ndani ya kisiwa cha Pemba.

Siti Rashid Salim (39), ambae kwa sasa ni ameshatalikiwa na aliekuwa mume wake miaka minne iliopita, aliamua kujiingiza kwenye biashara ya duka akiamini kuwa huko ataagana na umaskini.

“Naam biashara ya vyombo, juisi, soda na vitafunwa ilinikubwali kisawa sawa na mimi nilishaagana na umaskini, na maisha yangu yalikuwa juu na nikawa mwanamke wa kutegemewa na familia’’,anihadithia.

Siti alienza biashara hiyo miaka minne iliopita, alilinunua duka hilo kutoka kwa mwanajeshi mmoja, ambae yeye alipata uhamisho na kuhamia kisiwani Unguja kikazi.

Ndipo alipojitokeza yeye kuchukua nafasi ya kuendeleza duka hilo, na kujikusanyia idadi ya wateja wafikao 40 wa siku moja, na wakati akifunga duka mishale ya saa 3:30 usiku mapato hakuyaamini.

“Mimi ilikuwa nahesbu mauzo, na kisha najikuta na shilingi 150,000 hadi shiingi 160,000 na hapo sasa familia ilianza kuniangalia kwa jicho la utajiri’’,alifafanua.


Nikizungumza nae kwenye duka lake eneo la Wawi, kwa muda wa saa moja bila ya kupokea mteja kutokana na kugomewa kwa sababu ya chama anachokishabikia, anasema sasa yeye na umaskini yuko karibu mno mithili ya meno na ulimi.

“Ahaa…duka limekuwa limejaa hadi bidhaa nyengine kama chupa za chai zilikuwa nimezipanga chini hadi nje barazani, sasa unaona kama lililoingia moto, hakuna liwalo na umaskini umeshanipiga mbeleko’’,alinieleza kwa huzuni.

Ubeleko kwa Pemba ni mtu kumchukua na kumuweka mgongoni, ndiovyo mjasiriamali huyu, anavyojifafanisha yeye na kurejea tena kwenye umaskini, baada ya kubaguliwa na wanakijiji wenzake.

WAFUASI WA LIPUMBA KUTUA KWA MSAJILI WA VYAMA


Patricia Kimelemeta na Jonas Mushi, Dar es Salaam

WAFUASI wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, wametangaza kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuwasilisha malalamiko yao ya kupinga utaratibu uliofanywa na wajumbe wa Mkutano Mkuu cha chama hicho.

Wakati wanachama hao wanaomuunga mkono Prof. Lipumba wakidai hayo, CUF imetoa msimamo wake na kusema kuwa imeshamalizana na kiongozi huyo na kilichobaki sasa ni kujiandaa kujaza nafasi za uongozi zilizo wazi.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Salim Bimani, ilieleza kuwa wajumbe wengi wa Mkutano Mkuu Maalumu uliofanyika juzi walipiga kura ya kuridhia kujiuzulu kwa Prof. Lipumba na kwamba mchakato wa kujaza nafasi hizo utafanyika.

“Ni muhimu kukumbuka kwamba ajenda ya kwanza ya msingi katika Mkutano Mkuu imekamilika kwa wajumbe wengi kukubali kujiuzulu kwa mheshimiwa Prof. Lipumba.

WANAFUNZI 9 WALAZWA KWA MSHTUKO WA MABOMU

BAADHI ya waandishi wa habari kisiwani Pemba, wakifanya mahojiano na baadhi ya wanafunzi walifikishwa hospitali ya Chake Chake baada ya kupata mshtuko ya uripuaji wa mabomu, yaliyofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama kisiwani Pemba, katika mji wa chake chake leo asubuhi
MMOJA wa Wanafunzi wa skuli ya Madungu Sekondari waliolazwa katika hospitali ya chake chake baada ya kupata mshtuko wa uripuaji wa mabomu yaliyofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama mkoa wa kusini Pemba, katika maeneo mbali mbali ya Mji wa Chake Chake

BAADHI ya wanafunzi wakiwa ndani ya hospitali ya chake chake, sehemu ya mapokezi ya wagonjwa baada ya kuiwafikisha wanafunzi wenzao kupatiwa matibabu, kutokana na mshtuko walioupata kufuatia uripuaji wa mabomu yaliyofanywa na vikosi vya ulinsi na usalama Mkoa wa Kusini Pemba, katika maeneo mbali mbali ya mji wa chake chake
BAADHI ya Wanafunzi wa skuli ya Sekondari Madungu na Shamiani Chake Chake Pemba, wakiwa nje ya hospitali baada ya kurudi kuwafariji wanafunzi wenzao tisa, waliopata mshuko wa mabomu yaliyokuwa yakipigwa na vikosi vya ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba, katika maeneo ya mji wa Chake Chake asubuhi ya leo.(Picha zote na Thureya Ghalib, PEMBA.)

Monday, August 22, 2016