dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 21, 2014

Mawakili walalamikia washtakiwa wa ugaidi Z`bar kushtakiwa Kisutu

SHEIKH FARID APANDA MAHAKAMA YA KISUTU KWA UGAIDI

Na Rahma Suleiman
 
Mawakili wa watuhumiwa waliopo kizuizini kutokana na tuhuma za makosa ya ugaidi kutoka Zanzibar, wamedai kuwa kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwapeleka Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam ni kuidhalilisha Zanzibar kisheria.

Mawakili hao wakiongozwa na Abdallah Juma walitoa madai hayo mbele ya Jaji  Mkusa Isack Sepetu wa Mahakama Kuu Zanzibar wakati wakiwasilisha hati ya maombi ya dharura kufuatia wateja wao waliokamatwa Zanzibar na kupelekwa Tanzania Bara kushtakiwa.

Alidai watu hao wamenyimwa uhuru wao wa kikatiba kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 14 (1) (2) na kifungu cha 16 (1).

Alidai kuwa kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi cha kuwaweka kizuizini wateja wao kwa mienzi miwili sasa tena nje ya Zanzibar wakati Zanzibar ni nchi, ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 28 sheria namba 7 ya mwaka 2004 ya Zanzibar.“Zanzibar ni nchi tena ina mahakama yake kwa nini wateja wetu wakamatwe Zanzibar wakawekwe katika kizuizi kisicho halali Tanzania bara, hivyo jaji huoni kitendo hicho ni kuidhalilisha  mahakama yako tukufu,” alidai Abdallah Juma.

Aliongeza kuwa wateja wao wanne walikamatwa na polisi Zanzibar miezi miwili iliyopita kwa kuhusishwa na tukio la mlipuko wa bomu uliotokea eneo la Darajani Juni 13, mwaka huu na kuua mtu mmoja na majeruhi tisa.

Alisema kwa mujibu wa sheria za Zanzibar tukio limefanyika Zanzibar, hivyo watu hao wangepaswa kuhukumiwa katika mahakama za Zanzibar na siyo Dar es Salaam.

Aliendelea kudai kuwa wateja wao hawajapewa fursa ya kusikilizwa na kuiomba mahakama hiyo kufuata sheria.

Hata hivyo, upande wa mashitaka uliiomba mahakama kutupilia mbali madai hayo na Jaji Sepetu aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28, mwaka huu mahakama hiyo itakapotoa maamuzi kuhusiana na maombi hayo.

Watuhumiwa hao waliokamatwa  miezi miwili iliyopita kutokana na kosa la ugaidi ni  Nassor Hamad Abdallah, Mohammed Ishaq Yussuf, Said Kassim Ali, Hassan Bakari Suleiman, Rashid Ali Nyange, Antar  Humoud, Khamis Salum Amour na Salum Ali Salum.

Source: Nipashe

No comments :

Post a Comment