dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 26, 2014

Nyangumi Akutwa Ufukwe wa Pemba kijiji Shamiani

 Wafanyakazi wa Uvuvi pemba wakimpima Nyangumi alieonekana Pemba akiwa ameaguka ufukwe wa bahari wa shamiani.

Wananchi wakikata minufo ya Nyangumi aliyeangukia katika ufukwe wa bahari ya Pemba maeneo ya shamiani, kama wanavyoonekana pichani wakiwa katika harakati hizo.
Nyangumi aliyepwerewa katika ufukwe wa bahari ya Pemba Wilaya ya Mkoani akiwa na urefu wa mita 45  na upana mita 25 akiwa mkatika ufukwe wa shamiani Pemba wananchi wakikata mapande ya mnofo wake.

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Nyangumi huyu wananchi wakifanya kazi yao kukata minofo ya nyangumi huyu kwa ajili ya kupata mafuta ya nyangumi.




Nyangumi apwerewa Shamiani Pemba

Na Mwandishi Wetu. Pemba.
Katika hali isio ya kawaida huko maeneo ya bahari ya Shamiani (kwa gombe) jimbo la kiwani mkoa wa kusini Pemba kumeibuka kiumbe kikubwa cha ajabu kutoka baharini ambacho kimepwewa.

Kwa mujibu wa taarifa toka kwa baadhi wakaazi wa maeno ya jirani na eneo hilo ambao wamefurika kwa wingi kwenda kuona kiumbe hicho wamesema kuwa ni mara ya kwanza kuona kiumbe cha namna hio kikiwa kimepwewa ndani ya ba
hari.
Baadhi yao wameleza kuwa huenda pengine kiumbe hicho cha ajabu chenye urefu takribani mita 40 na upana zaidi ya mita 25 kikawa ni samaki aina ya nyangumi au chongowe.
Katika hali ya kushangaza ndani ya fukwe hizo za bahari ya kwa gombe watu zaidi ya 200 kutoka maeneo jirani ya likoni,mwambe na ngambu shamiani wamejitokeza kuona kiumbe hicho cha ajabu ambacho tayari kimekufa.
Aidha makundi ya wananchi wanaendelea kukata minofu ya aina hio ya kiumbe huku wengine wakijaza madumu yao mafuta yanayotiririka kutoka kwa kiumbe hicho.
Kwa upande wake mtalamu wa viumbe vya bahari Zanzibar kwa masharti ya kutokutajwa jina amesema msimu huu viumbe vya bahari aina ya nyangumi hupita katika ukanda wa bahari ya hindi.

‘’Inaonekana baadhi ya watu huwapiga aina hii ya viumbe vya bahari ndio maana hufariki dunia,hali hii inaitia nchi yetu jina baya kimataifa kuonekana tunawauwa kwa makusudi’’aliongezea mtaalamu huyo.
Alieleza kuwa kitengo chao kimeshatoa elimu sana ili wananchi waache tabia hii ya kuwangamiza viumbe hawa kwani dunia haikubali kwa sasa kwa vile ni viumbe adimu na muhimu. 
Aidha alieleza jumuaya (Skubado) inaweza kutubana kwa jambo hili na ameshauri wananchi ikitokezea wamemuona kiumbe aina hii kipo hai basi watoe taarifa kwa wahusika ili aweze kurudishwa baharini.
Hali hii ya kuonekana kiumbe cha ajabu ni mara ya kwanza kwa maeneo haya ambapo kumeibua mshangao mkubwa kwa wananchi mbali mbali wa maeneo haya.
Chanzo: ZanziNews

No comments :

Post a Comment