dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 26, 2015

Wabunge, wasomi wamshupalia Muhongo.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
Wabunge kadhaa wametoa maoni tofauti kufuatia kujiuzulu kwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo juzi.
Mbunge  wa Mwibara (CCM), Kange Lugora, alisema kuwa  kujiuzulu kwake ni kutimiza agizo la Bunge badala ya kumsubiria Rais Jakaya Kikwete amwajibishe.
Lugora alisema sakata la Escrow limewapunguzia ushindi kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa kwa kuwa wapinzani walikuwa wanalitumia kama mtaji na fimbo ya kisiasa.
Mbunge wa  Kuteuliwa ( NCCR-Mageuzi), James Mbatia,  alisema sakata la Escrow linaendelea kuligharimu taifa kutokana na serikali kutokufanya maamuzi sahihi na kwa wakati.
 “Muhongo amefukuzwa siyo kwamba amejiuzulu tulishamfukuza na bungeni tulipopitisha maazimio tangu Novemba mwaka jana,” alisema Mbatia.
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, alisema alichokifanya  Muhongo si kitendo cha kishujaa kwani ameshinikizwa.
Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo  Filikunjombe, alisema sababu ambazo amezieleza Waziri Muhongo alitakiwa kuzitoa wakati wa mjadala kwani siyo mpya.
Kwa upande wake Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, alisema Rais Kikwete, ameonyesha udhaifu katika kutekeleza maazimio ya Bunge kwa sababu alipaswa kumfukuza kazi Waziri Muhongo badala ya kumuacha ajiuzulu.
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari, alisema Muhongo asipowatajia wezi hawatamruhusu kuchangia chochote bungeni kwa sababu hatakuwa na uhalali.
Alisema kwa sasa Muhongo ameondoka kwenye upande wa serikali na kubaki kama mbunge, hivyo anakuwa ni sehemu ya maazimio ya Bunge.
" Tunaomba aturahisishie kazi ya Bunge kujua fedha zetu ziko wapi, ni kina nani wengine waliohusika, na atueleze ni kina nani waliochota fedha kupitia Benki ya Stanbic, vinginevyo bado hana uhalali wa kuwapo bungeni," alisema Nassari. 
Mhadhiri wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Maina Peter, alisema kujiuzulu ni jambo jema lakini limechelewa. 
Alisema Muhongo angeheshimu demokrasia angejiuzulu hakutakiwa kuendelea kushikilia kiti kwani imekuwa kama aibu.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment