dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 4, 2015

Kapteni Komba aacha historia.

Aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), Kapteni mstaafu John Komba.
Aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), Kapteni mstaafu John Komba, amezikwa katika kijiji cha Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma huku akiacha historia kutokana na mazishi yake kuhudhuriwa na umati wa watu wakiwamo viongozi waandamizi wa serikali na vyama vya siasa.
 
Rais Jakaya Kikwete jana aliongoza viongozi na wananchi walioshiriki katika mazishi hayo yaliyofanyika saa 10:00 jioni katika kijiji hicho .
 
Mbali na Rais Kikwete, viongozi wengine waliohudhuria mazishi ya Komba ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya.
 
Wengine ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mkangara; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenister Mhagama; Spika wa Bunge,  Anne Makinda; Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa CCM, abdulrahman-Kinana. Kabla ya mazishi kufanyika, shughuli ya kuaga mwili zilifanyika katika Shule ya Msingi Lituhi.
 
Mamia ya wananchi walipata fursa ya kuuaga mwili wa Kapteni Komba ambaye pia alikuwa mhamasishaji mkuu wa CCM kupitia kikundi chake cha Tanzania One Thietre (TOT) ambacho alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wake.
 
Wakati wa kuaga mwili huo, watu kadhaa walianguka kwa kupoteza fahamu na kuangua vilio hali iliyofanywa watoa huduma ya afya kufanya kazi ya ziara kuwapatia huduma ya kwanza.
 
Baada ya mwili wa Kapteni Komba kuwasili, simanzi na vilio  vilivyotawala na wakati wa kuuaga  katika viwanja vya Shule ya Msingi Lituhi ambako  alisoma elimu ya msingi na baadaye kuzikwa kwenye makaburi ya familia.
 
Ibada ya mazishi iliongozwa na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, Mhashamu John Ndimbo.
 
Wakizungumza na NIPASHE  wakati wa kuuaga mwili huo, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lutuhi walisema wanasikitishwa na kifo cha mbunge wao ambaye alikuwa anawajali na kwamba wanaweza wasipate mbunge mwingine  ambaye atawasaidia kama alivyokuwa akifanya Kapteni Komba.
 
Joseph Thawalla, mkazi wa kijiji hicho,  alisema kifo hicho kimeleta mshtuko kwa kijiji kizima na wananchi wa jimbo lake ambao bado walikuwa wakimtegemea.
 
Alisema Kapteni Komba alikuwa Mbunge, ambaye alikuwa akijitoa kwa wananchi wake kuwasaidia hata wakati alipokuwa akihudhuria mikutano ya Bunge.
 
Alisema  alipokuwa akisikia jambo baya limewapata wananchi wake, alikuwa akiacha vikao vya Bunge na kwenda kuwaona jimboni kwake.
 
“Jimbo letu ili lizidi kuwa na maendeleo zaidi, tunahitaji Mbunge atakayetujali na kushirikiana na sisi katika shughuli za maendeleo,” alisema Thawalla.
 
Kwa upande wake, aliyekuwa Katibu wa Kapteni Komba,  Charles Mackenzie, alisema Marehemu alikuwa akijali wananchi wake na alifanya nao kazi kwa moyo na kwamba wananchi walimkubali.
 
Alisema alikuwa akijali shida zao na mara nyingi alikuwa akijitoa kuwasaidia kuanzia mtu mmoja mmoja, vikundi na taasisi.
 
Mackenzie alisema Kapteni Komba alikuwa ameahidi mabati kwenye kila shule ya sekondari ya kata katika jimbo lake na tayari 1,000 na nondo vilikuwa vimeagizwa kuelekea kijijini hapo.
 
“Mabati 1,000 na nondo mbunge alikuwa ameviagiza, viko mjini vinakuja huku, “ alisema.
 
WABUNGE WATOA RAMBIRAMBI
Wabunge wa Mkoa wa Ruvuma walitoa mkono wa pole wa Sh. milioni tatu kwa familia ya marehemu Kapteni Komba.
Kapteni Komba alifariki dunia Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
  
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment