dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 27, 2015

Mansour aunga mkono msimamo wa Moyo

Image result for mansour yussuf himid

Zanzibar. Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mansour Yussuf Himid amesema msimamo wa mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo kuendelea kutetea mamlaka kamili ya Zanzibar ndani ya mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa kishujaa licha ya kufukuzwa CCM.

Mansour aliyefukuzwa CCM mwaka 2012 kwa madai ya kwenda kinyume na miiko na maadili ya chama, amekuwa wa kwanza kujitokeza na kumuunga mkono Moyo kwa msimamo wake kuendelea kupinga Muungano wa serikali mbili.
Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Arabama Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mansour alisema pamoja na Moyo kuwa na mchango mkubwa katika harakati za historia ya ukombozi wa Zanzibar na CCM, bado amendelea kubakia imara tangu alipofukuzwa ndani ya CCM Aprili 19.
Alisema anaunga mkono msimamo wa kudai mamlaka kamili ya Zanzibar katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu mfumo wa serikali mbili umekuwa ukiinyonya Zanzibar na kusababisha kushindwa kujiamulia mambo yake ya kiuchumi na kisiasa.
“Napenda kutumia nafasi hii kumpogeza Mzee Moyo kwa ujasiri wake licha ya kufukuzwa na bado amendela kubakia imara bila ya kutetereka na wananchi tumuunge mkono,” alisema.
Akimzungumzia Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Haamad, Mansour alisema ni kiongozi hodari mwenye msimamo kwa masilahi ya Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu alisema Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), imeanza kazi kwa kuchechemea kwa vile imeshindwa kutangaza mipaka ya majimbo licha ya kazi ya ukaguzi mipaka kukamilika.

No comments :

Post a Comment