dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 25, 2015

Joto la uchaguzi lapanda


  • Vyama vyapigana vikumbo majimboni kusaka wagombea, wapigakura, mawakala.
Dar es Salaam. Joto la Uchaguzi Mkuu limezidi kupanda, baada ya baadhi ya vyama vya siasa kuanza harakati za kuwatafuta wagombea, wapigakura na mawakala katika majimbo mbalimbali nchini.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa takriban kila chama kinachojipanga kusimamisha wabunge, kipo kwenye harakati ya kujiweka sawa kwa namna mbalimbali.
Wakati Chama Cha Wananchi (CUF), kikianza mchakato wa kura ya maoni na kuzunguka mikoani kuwahamasisha watu wajiandikishe kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura, Chadema imetangaza kutolewa kwa fomu za kuomba kugombea ubunge na udiwani na CCM kimejichimbia Dodoma kutoa ratiba ya uchaguzi.
Kwa upande wake NCCR-Mageuzi kimeshapiga kipenga cha kuchukua fomu za Ubunge na Udiwani, ACT Wazalendo kilipanga kukutana wiki iliyopita kujadili uchaguzi na Alliance for Democratic Change (ADC), kinaendelea na ziara zake mikoani.
CUF
Chama cha Wananchi (CUF) kimeanza ziara katika mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi, Shaweji Mketo aliliambia gazeti hili kuwa ziara hiyo ya siku kumi, inafanywa na makundi matatu yaliyotawanyika katika mikoa mbalimbali ikiwamo mkoani Tabora ambako Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahim anaongoza.
“Tumeanza ziara yetu leo (Ijumaa) iliyopita katika mikoa ya Tabora, Kagera, Singida, Shinyanga na Dodoma. Mwenyekiti anaanzia mkoa wa Tabora,” alisema Mketo.
Chadema
Chadema tayari kimeruhusu makada wake wanaotaka kugombea ubunge na udiwani kujitokeza kuchukua fomu, huku mgombea urais wa chama hicho akipangwa kujulikana Agosti 4, mwaka huu.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wake, kimejichimbia Dodoma kwa ajili ya vikao vyake ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alieleza kuwa pamoja na kujadili masuala mengine, vikao hivyo vimepanga ratiba, kanuni na taratibu za Uchaguzi Mkuu na tayari makada sita waliokuwa wamefungiwa wamefunguliwa.
Joto hilo la Uchaguzi Mkuu pia linaendelea kupanda ndani ya Chama cha CCR-Mageuzi ambako makada wake nao wamesharuhusiwa kuchukua fomu za kuwania nafasi za udiwani, ubunge na Urais. Tayari Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk George Kahangwa ameshachukua fomu kwa ajili ya kujitosa kuwania nafasi hiyo.
Pia Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, ilikutana wiki iliyopita kujadili masuala ya Uchaguzi Mkuu pamoja na mambo mengine, ikiwamo utaratibu wa uchukuaji wa fomu za kugombea  nafasi mbalimbali.
“Katika mkutano huo, ajenda kubwa itakuwa ni kuidhinisha uteuzi wa Manaibu Katibu Mkuu, kuteua Makatibu wakaounda Sekretariati, kupitisha mkakati wa chama kuelekea Uchaguzi Mkuu,” alisema msemaji wa chama hicho, Abdallah Hamis alipozungumza na gazeti hili mwishoni mwa juma.

No comments :

Post a Comment