dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 25, 2015

Mbowe: Ndoto ya Nyerere kutimia Oktoba


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam jana. Picha na Anthony Siame 
  • Mbowe aliyasema hayo jana katika mkutano wa chama wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam ambako pamoja na mambo mengine alizindua kitabu cha mambo aliyoyafanya mbunge wa jimbo hilo, Halima Mdee na wimbo maalumu wa msanii wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha.
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema matamanio ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya kuwaletea Watanzania mabadiliko waliyoyakosa ndani ya CCM yanaenda kutimia katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Mbowe aliyasema hayo jana katika mkutano wa chama wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam ambako pamoja na mambo mengine alizindua kitabu cha mambo aliyoyafanya mbunge wa jimbo hilo, Halima Mdee na wimbo maalumu wa msanii wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha.
Akizungumza katika mkutano huo uliorushwa moja kwa moja na ITV, Mbowe alisema katika maeneo yote ya nchi, watu wamekata tamaa ya maisha kutokana na uongozi mbaya wa chama tawala, hivyo wako tayari kufanya mabadiliko ya mfumo wa utawala.
“Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu matamanio ya Mwalimu Nyerere yanaenda kutimia. Watanzania wanataka mabadiliko ambayo wameyakosa ndani ya CCM. Nimezunguka nchi nzima na kubaini kuwa wananchi wanazo sababu na uwezo wa kuyaleta mabadiliko kutokana na kiu waliyonayo,” alisema.
Mbowe aliyeanza mkutano huo kwa kukagua gwaride la kikundi cha Red Brigade, alitoa kauli hiyo akimnukuu Mwalimu Nyerere aliyepata kusema kuwa, “Watanzania wanataka mabadiliko. Wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.”
Alitumia fursa hiyo kuzungumzia mchakato wa uandikishaji wapigakura kuwa unahitaji kutazamwa kwa namna nyingine ili kuwatendea haki wananchi ambao wana shauku ya kutimiza haki hiyon ya kikatiba.
“Juzi nilikuwa Mbeya, nimeshuhudia wananchi wakilala katika vituo vya kuandikishia kutokana na hofu waliyonayo kukosa uchaguzi mkuu. Namkumbusha Jaji Lubuva (Damian, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi) aongeze muda na isiwe siku saba kama ilivyopangwa awali. Kutofanya hivyo atakuwa anajitafutia lawama ambazo hakutakuwa na kiongozi yeyote wa CCM atakayesimama kumtetea pindi wananchi watakapokuwa wanamlaumu hapo baadaye,” alisema.
Mwenyekiti huyo mwenza wa umoja wa Katiba ya wananchi (Ukawa), pia alibainisha mkakati wa umoja huo kugomea na kuipinga rasimu inayotaka vyombo vyote vya habari kujiunga na Shirika la Habari Tanzania (TBC) kwa taarifa ya habari ya saa 2.00 usiku.
“Tutaleta vurugu. Tutasimamisha Bunge kupinga sheria hiyo kwa sababu hiyo ni hujuma ambayo wananchi hawaikubali na mimi kama kiongozi wa upinzani nitalisimamia hilo,” alieleza.
Akimakaribisha Mbowe, Naibu Katibu Mkuu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alisema mkutano huo ni muhimu na chama kimeuandaaa ili kuthamini umuhimu wa wanawake katika jamii.
“Mwenyekiti fikiria kama wewe unabeba mimba miezi tisa, ujifungue na kumlea mtoto. Hayo ndiyo wanayoyafanya wanawake hawa. Ni lazima tukubali ujasiri wao kwa kuyajali majukumu yao,” alisema Mnyika.
Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani, Mabere Marando alisema Chadema kimejipanga kuwaleta viongozi wake wote jijini hapa kufanya kampeni ya uandikishaji katika daftari la kudumu ili wapigakura wafike milioni 3.5 na kuiondoa CCM madarakani.
“Nimepokea malalamiko kutoka kwa askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambaye analipwa Sh22,000 kwa mwezi. Anaamini Chadema itamtendea haki ili kipato chake kiweze kukidhi mahitaji,” alisema Marando.
Mkutano huo pia ulizindua kikosi cha Red Brigade ambao wapo 200 katika kila jimbo nchini, wakiwa na jukumu la kulinda kura katika vituo vyote kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Gwajima ahutubia
Katika mkutano huo, Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, mwimbaji Flora Mbasha pamoja na mumewe Emmanuel Mbasha ni miongoni mwa wageni walioalikwa katika mkutano huo.
Baada ya Mbowe kuhutubia, mashabiki walipiga kelele wakitaka Askofu Gwajima naye ahutubie.
Askofu huyo alipopewa nafasi alisema kiongozi anapokaribia kupoteza madaraka Mungu humpa ukichaa na kuacha kuona matatizo ya watu.
“Kwa hali ilivyo sasa, viongozi wa Serikali wamepewa ukichaa, hawanaoni matatizo ya watu. Muda wa mabadiliko ndio umewadia, alisema.
Bavicha watishia
Awali, Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) lilieleza dhamira ya kufanya maandamano kuishinikiza NEC kama haitaongeza muda wa kuandikisha wapigakura.
Katibu Mkuu wa Bavicha Taifa, Julius Mwita alieleza hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa kata wa chama hicho katika Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam.
“Kwa mijibu wa ratiba ya Tume, uandikishaji utafanyika kuanzia Julai 4 mpaka 16. Dar ina wakazi zaidi ya milioni nne, je, muda huo unatosha kuwafikia watu wote wanaostahili kuandikishwa? Kama hautoshi basi tuishinikize Tume kuongeza muda huo,” alisema Mwita.

Aliongeza endapo hilo halitafanywa Bavicha itaandaa maandamano ili kuishinikiza watu wote wenye sifa waaandikishwe.
Katibu mkuu wa mstaafu wa Bavicha, Deogratias Munishi aliwataka viongozi hao kujiamini katika kufanya maamuzi na kusisitiza kuwa kila kizazi kina utume wake, hivyo matazamio ya Watanzania yapo kwao.
“Wananchi wanataka kuona maisha yao yanakuwa bora kwa kupata elimu bora, afya pamoja na chakula cha uhakika. Hayo yote Chadema inaweza kuyafanikisha na ninyi ndiyo wahusika wa kuwasikiliza,” alisema.

No comments :

Post a Comment