dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, May 23, 2015

WAWILI WASHIKILIWA KWA KUMTUKANA DK. SHEIN NA MAKAMU WAKE!

   
JUU NI SAID ALI ABDALLAH ANAESHIKILIWA NA POLISI. 
(ANGALIZO: VIDEO HAIJAWEKWA NA NIPASHE)

NA RAHMA SULEIMAN

23rd May 2015

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein
Polisi Zanzibar inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuwatukana na kuwakashifu viongozi wakuu wa serikali, akiwamo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makao makuu ya Jeshi la Polisi visiwani hapa, Naibu Mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI), Salum Msangi, alisema watu hao wapo chini ya ulinzi  mpaka  hapo upelelezi utakapokamilika ili wafikishwe mahakamani. Aliwataja watu hao ambao ni wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kuwa ni Said Ali Abdallah (26), aliyetoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar na Makamu wa Pili wa Rais na watendaji wa jeshi la polisi.
Alisema mtuhumiwa huyo alitoa maneno hayo na kusambaza vitisho katika mitandao ya kijamii akisema endapo mwaka huu katika uchaguzi mkuu CUF haitashinda, watachoma kambi na nyumba za jeshi hilo kisiwani Pemba.
Alimtaja mtuhumiwa mwingine kuwa ni Hussein Mageni Hussein, maarufu Beko (27),  ambaye alimpigia simu Balozi Iddi na kumtukana na kumtumia ujumbe wa simu wenye maneneo ya kashfa.
“Katika ujumbe wa sauti uliokuwa ukisambazwa na mtuhumiwa Said Ali Abdallah alitoa onyo kwa viongozi wakuu akimtaka rais wa Zanzibar na makamo wa pili wa rais wasiende Pemba kwani hakuna wafuasi wa chama chao na kudai kuwa chama anachokishabikia ambacho ni CUF kisiposhinda kwenye uchaguzi mkuu ujao atahamasisha wafuasi wezake wazitambue nyumba za askari polisi na waziteketeze familia za askari hao,” alisema.
Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa kisiwani Pemba Mei 20, na kuonekana kuwa watuhumiwa hao ni wahalifu wa kawaida wasio na msukumo wa viongozi wa vyama vya siasa katika ushabiki wao.
Alisema baada ya kuwakamata watuhumiwa hao jambo lililowashangaza, baadhi ya viongozi wa CUF na wanasheria wamekuwa mstari wa mbele kuwashambilia wahalifu hao.
Alisema baada ya mtuhumiwa Said Ali kufikishwa makao makuu ya polisi Zanzibar, Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani, Hija Hassan Hija (CUF), akiwa na mawakili watatu wa chama hicho walifika na kuanza kumtetea mtuhumiwa huyo hata kabla hajaanza kuhojiwa.
Alisema hali hiyo inatoa picha kuwa watuhumiwa wanashawishiwa na viongozi wa  CUF wakishirikiana na mawakili ili kuvuruga amani ya nchi. Alisema uchunguzi wa awali, umebaini kuwa watuhumiwa wametenda makosa hayo kwani hata mawasiliano ya simu waliyokuwa wakitumia yalichunguzwa na kujulikana ni wao na maeneo wanayoishi.
“Simu walizokuwa wakitumia ni za mtandao wa Zantel na tulifuatilia hadi katika kampuni ya mtandao huo na tukawabaini,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment