dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 28, 2015

SIO GHARIKA, SIO MAFURIKO, SIO SUNAMI, BALI NI KIAMA JANGWANI LEO JUMAAMOSI (ASTAGHFIRULLAH)!

Default Sio gharika, sio mafuriko, sio sunami, bali ni kiama jangwani leo jumaamosi!

 By JF Senior Expert Member
Mapema jana Ijumaa nilipiga simu nyumbani Kibirinzi, Chake Chake, Pemba, ili kuwapa hongera kwa kiwanja cha watoto kufunguliwa rasmi na Rais Dr Shein, mara nikapewa nizungumze nae rafiki yangu wa zamani ambae anaishi DSM kaenda nyumbani kwa weekend. La mwanzo nikamuuliza, je, umekimbia GHARIKA ya kesho (yaani leo Jumaamosi) huko Jangwani? Akaniambia kuwa….”sio gharika, sio mafuriko na wala sio sunami, bali itakuwa ni KIAMA hio kesho huko Jangwani, kwani watu mara 5 ya wale waliofika kwenye ufunguzi wa kampeni ya CCM wanategemewa kufika”. Nilikata simu hapo hapo na kuanza kufikiria huyu Lowassa anakitu gani cha zaidi cha kuwavutia wananchi kama hivi? Najua jibu nitalipata hio tarehe 25 October, 2015 na kwa sasa msinijibu kitu!

No comments :

Post a Comment