dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 3, 2015

Wasira aibuka kidedea Bunda.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira, ameshinda kwenye kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (ccm), katika jimbo la Bunda mkoani Mara baada ya kupata kura 6,429 na kumshinda mpinzani wake wa karibu ambaye ni mjasiriamali Robert Maboto aliyepata kura 6,206.
Akitangaza matokeo hayo jana Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda, Magreth Mtatiro, alisema kuwa Wasira ameshinda katika kinyang'anyiro hicho kwa zaidi ya kura 223 kati ya kura zote zilizopigwa 16, 262.
Mtatiro alimtangaza mshindi wa tatu kuwa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya (1,140), Exavery Lugina (846), Simon Odunga (547), Magesa Mugeta (446), Peres Magiri (385) na Burian Bitaa (263).
Alisema kutokana na matokeo hayo, alimtangaza  Wasira kutetea tena ubunge katika jimbo hilo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini Oktoba 25, mwaka huu. 
Alisisitiza  kuwa matokeo hayo ni halali kwa sababu kila mgombea aliweka wakala wake kwenye kituo cha kupigia kura.
“Tulikuwa na wagombea wanane katika jimbo hili la Bunda mjini na kila mgombea alikuwa ameweka wakala wake kwenye kituo cha kupigia kura na wameridhika na matokeo haya,” alisema katibu huyo wa CCM wilayani Bunda.
Kwa upande wake Wasira, alishukuru wanachama wa chama hicho waliompigia kura, wale ambao hawakumpigia kura na wananchi walioijitokeza kufuatilia matokeo hayo, akisema kuwa ushindi huo ni wa wanaCCM wote nchini.
Alisema kuwa mshindi kamili atapitishwa na vikao vya juu vya chama hicho kama ilivyo kawaida kwa kufuta kanuni na taratibu.
Wasira aliwaomba wagombea wengine katika jimbo hilo kuvunja kambi zao na kuwa kitu kimoja baada ya uchaguzi huo wa kura za maoni kwisha ili chama hicho kipate ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo utakaovishirikisha vyama vingi vya siasa.
ILEMELA
Angelina Mabula (6,324), Barnabas William (3,562), John Lupemba (1,167), Stephen Mirimi (1,064) na Godwin Gondwe (827). 
NYAMAGANA
Stanslaus Mabula (9,553), Joseph Kahungwa (3,647), Raphael Shilatu (864), Robert Masunya (830) na Dede Petro (443).
SHINYANGA MJINI
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga, Charles Sangula, alisema katika jimbo la Shinyanga mjini, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Steven Masele, amepata ushindi wa kishindo katika kura za maoni zilizofanyika juzi.
Sangula akitangaza matokeo hayo, alisema kura Masele ameibuka mshindi kwa kupata kura 7,900, Dk. Charles Mlingwa (669), Erasto Kwilasa (232) na Tara Mzeimana (43).
KISHAPU
Suleiman Nchambi
SOLWA
Ahmed Salimu
MSALALA
Ezekiel Maige
KAHAMA
Jumanne Kishimba
USHETU
Elias Kuandikwa
BUKOBA
Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki, ameshinda kura za maoni kuwania ubunge kupitia CCM baada ya kuwashinbda wapinzani wake wanane.
Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini, Ramadhan Kambuga, alisema hayo wakati akitangaza matokeo ya kura hizo kwa waandishi wa habari.
Alisema Kagasheki ameibuka mshindi baada ya kupata kura 6,971, Dk. Anatory Amani (944), George Rubaiyuka (113), Josephat Kaijage (71), Mujuni Katarahiya (53), Philbert Katabazi (34), Celestina Rwezaura (29) na Elieth Lukomoka (19).
CHATO
 Katibu wa CCM Wilaya ya Chato, Hamis Mkaruka, alisema Dk. Medard Kalemani ameshinda kwa  12,892, Deusdedith Katwale (3,251), Simon Bulenganija (2,150)
 BUSEGA
Dk. Titus Kamani (10,697), Raphael Chegeni (9,661).
BARIADI
Andrew Chenge (20,020), Masanja Kadogosa (2,986)
ITILIMA
Daudi Njalu (44,486), Simon Ngangani (2,759), Dhan Makanga (814)
MEATU
Salum Mbunzi (13,180), Oscar Maduhu (2,988), Romano Thomas (358).
KISESA
Luhaga Mpina (hakuwa na mpinzani)
TABORA
Emmanuel Mwakasaka (11,280), Ismail Aden Rage (3,380)
IGALULA
Mussa Ntimizi (7,200), Dk. Athuman Mfutakamba (3,500) na Hanifa Kitwana Kondo (3,200), hata hivyo kura hizo bado zinajumlishwa.
TABORA KASKAZINI
Almas Maige (9,000), Shafin Mamlo Sumar (6,000) na Joseph Kidaha (5,000), kura zilikuwa zinaendelea kuhesabiwa.
ULYANKULU
John Kadutu kura 13,600, Dk. Msonde Syden (1,167) na Prof. Juma Kapuya.
URAMBO MASHARIKI
Magreth Sitta (12,392) na Ali Maswanya kura 4,175.
MANONGA
Seif Gulamali anaongoza hadi gazeti linaenda mitamboni.
BUKENE
Suleiman Zedi kura (12,894), Deo Kahumbi (2,728), Tedy Kaselabantu (1,441).
SIKONGE
Said Nkumba anaongoza kwa kura dhidi ya Rajab Kakunda.
NZEGA MJINI
Hussein Bashe anaongoza akifuatiwa na Joseph Ngulumwa.
NZEGA VIJIJINI
Dk. Hamis Kingwangallah anachuana kwa mbali na Lucas Selelii.
BUCHOSA
Dk. Charles Tizeba (26,368) na Eston Kasika (9,213).
RORYA
Lameck Airo kura 22,566

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment