dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 21, 2016

VITA KWENYE MKUTANO MKUU WA CUF!



By Peter Elias na Raymond Kaminyoge: mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Mkutano Mkuu wa dharura wa CUF umevunjika baada ya kundi la wafuasi wa chama hicho kuvamia na kufanikiwa kuzima mchakato wa kupiga kura kumchagua mwenyekiti mpya, wakishinikiza Profesa Ibrahim Lipumba aruhusiwe kurejea katika wadhifa huo.

Wafuasi hao wameingia ukumbini wakati wajumbe zaidi ya 700 wa mkutano huo wakijiandaa kupiga kura usiku huu kumchagua mwenyekiti, jambo lililozua vurugu zilizoambatana na uvunjaji wa viti na meza.

Kufuatia hali hiyo, mwenyekiti wa mkutano huo, Julius Mtatiro amelazimika kuahirisha uchaguzi mpaka utakapotangazwa tena.

Profesa Lipumba ambaye alijiuzulu wadhifa huo Agosti, mwaka jana baada ya kutofautiana na vyama vinavyounda Ukawa kwa kumpokea Edward Lowassa, alitoka nje ya ukumbi wa Blue Pearl ulikofanyika mkutano huo, huku akisindikizwa na vijana waliokuwa wakiimba nyimbo za kumsifu.







No comments :

Post a Comment