dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 25, 2016

JK ALIPOICHAGIZA DUNIA KUCHANGIA ELIMU MBELE YA MAELFU YA WAKAZI WA NEW YORK!

Rais Mstafu Jakaya Kikwete, na Kamishna wa Kamisheni ya Kimataifa kuhusu elimu akizungumza mbele ya umati wa wakazi wa jiji la New York katika tamasha la Global Citizen Festival lililofanyika Central Park. Kupitia tamasha hilo, Kikwete aliichagiza jumuiya ya kimataifa kuchangia na kuwekeza katika elimu kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na kijacho. Pamoja naye ni Makamishna wenzie, Waziri Mkuu wa Norway Erna Solberg na aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Australia Julia Gillad.
Umati wa wakazi wa jiji na New York waliojitokeza katika tamasha hilo fedha zinazopatikana kipitia tamasha hilo hupelekwa kusaidia masuala mbalimbali ya kijamii. Tamasha hilo lilitumbuizwa na wanamziki maafuru akiwamo Rihanna ambaye ametangazwa kuwa Balozi wa Elimu.
Rais Mstaafu Kikwete akisalimiana na Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power walipokutana kwenye tamasha hilo.
Rais Mstaafu akibadilishana mawili matatu na Waziri wa Mazingira wa Nigeria Amina Mohammed ambaye naye alikuwa mmoja wazungumzaji katika tamasha hilo

Na Mwandishi Maalum,New York

Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amasema, Afrika itandelea kubaki nyuma kielimu ikiwa jitihada za makusudi hazitafanyika kuwekeza katika elimu.

Ametoa kauli hiyo jana jumamosi mbele ya maelfu kwa mamia ya wakazi wa Jijini la New York waliofurika Central Park kuhudhuria tamasha maarufu lijulikanalo kama Global Citizen Festival.

Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka huwaleta pamoja viongozi kwa kada mbalimbali, wanaharakati na idadi kubwa ya waungaji mkono wa juhudi za kuutokomeza umaskini uliokidhiri na limeandalia na mtandao wa Uraia wa Kimataifa ( Global Citizen) kwa pamoja na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu Elimu ( Global Partnership for Education).

Aidha fedha zinazopatika kupitia tamasha hilo hutumika katika kusaidia masuala ya kimandeleo kama yakiwamo ya afya, elimu, mazingira, usalama wa chakula pamoja na masuala yanayohusu wanawake na watoto wa kike.Ni katika tamasha hilo ambalo mwaka huu limelenga pamoja na masuala mengine, fursa ya elimu kwa watoto wote ambapo, Rais Mstaafu Kikwete ambaye pia ni Kamishna katika Kamisheni ya Kimataifa kuhusu Elimu, ameitaka jumuiya ya kimataifa kupitia hadhara hiyo kusaidia na kuwekeza katika eneo hilo muhimu kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na kijacho.

“ Afrika yangu, itakuwa makazi ya vijana bilioni moja ifikapo mwaka 2050, na tayari ipo nyuma kielimu” akasema Kikwete na kuongeza. “Kama hatutawawezesha vijana wote sasa kwa kuwapatia ujuzi na maarifa , uchumi utapoteza kiasi cha dola 1.8 trilioni na watoto 800 milioni hawata kuwa shuleni ifikapo mwaka 2030. Na hii ni gharama ya kutoelimisha sasa”

Rais Mstaafu aliyezungumza na halaiki hiyo kwa pamoja na Makamishna wenzie, Waziri Mkuu wa Norway Bi. Erna Solberg na Waziri Mkuu wa zamani wa Australia, Bi. Julia Gillard ambaye ni pia ni Mwenyekiti wa Ushirikiano wa Kimataifaka kuhusu Elimu ( GPE).Amesisitiza kwamba “ Ni lazima tujenge kizazi kinachojifunza kwa kuogeza fedha kiasi cha dola 3 trilioni ifikapo mwaka 2030. Washirika wa maendeleo ni lazima waungane nasi katika misheni yetu hii, na sehemu kubwa ya fedha lazima zitoke katika vyanzo vya mapato vya ndani”.

Katika harakati hizo za kuwafikishia fursa ya elimu watoto wote wa kike na kiume, Global Partnership for Education and Global Citizen, wamemtangaza mwanamziki maarufu wa Marekani Rihanna kuwa Balozi wa Elimu ambapo kupitia Taasisi yake ya Clara Lionel watafanya kampeni ya pamoja na Global Partinship for education na Global Citizen kuhakikisha kwamba watoto wote wa kike na wa kiume wanapa fursa ya elimu bora.

Jukumu jingine la mwanamsiki huyo ni pamoja na kuwahamasisha viongozi wa dunia kuunga mkono uwekezaji katika elimu nchini mwao.

Rihanna na wanamziki wengine maaufu alitumbuiza katika tamasha hilo.

No comments :

Post a Comment