dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 21, 2017

Afariki dunia baada ya kuangukiwa na jiwe!

Mvua kubwa
MTU mmoja amefariki dunia kutokana na majeraha aliyopata baada ya kuangukiwa na jiwe lililokuwa limewekwa juu ya paa ili kulizuia lisiezuliwe na upepo, wilayani Manyoni, mkoani Singida.

Jiwe hilo lilimwangukia Kaundime Abrahaman (10) mapema wiki hii kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha usiku katika vijiji vya Makasuku na Chibumagwa katika tarafa ya Kilimatinde, wilayani Manyoni.

Mbali na kifo hicho, mvua hiyo pia ilisababisha watu wengine wanne kujeruhiwa, nyumba na majengo 107 kuezuliwa mapaa na mengine kubomoka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Debora Magiligimba, alisema Abrahaman alikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Makasuku.

Alisema mwanafunzi huyo aliangukiwa na moja ya mawe yaliyokuwa yamewekwa juu ya paa ili kulizuia lisiezuliwe na upepo na kumjeuhi.

Kamanda Debora alisema Abrahaman alipelekwa katika zahanati ya kijiji cha Chibumagwa lakini akafariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Kamanda, waliojeruhiwa na kutibiwa katika zahanati ya Chibumagwa ni Charles Ngaula (62), Gabriel Hugo (37 ), Julius Paul (57 ) na Mbereje Msangu ambaye umri wake haukupatikana mara moja, wote kutoka kijiji cha Makasuku.

“Nyumba 97 zilizoezuliwa ni za wananchi ambapo 92 ni za kijiji cha Makasuku na tano ziko katika kijiji cha Chibumagwa,” alifafanua.

Mbali na nyumba za wananchi, mvua hiyo pia iliharibu majengo saba ya serikali huku mawili yakiwa ya Idara ya Mahakama, alisema.
Katika kipindi ambacho pamekuwa na tahadhari ya kuwapo kwa upungufu wa mavuno, Kamanda huyo alibainisha kuwa mvua hiyo pia imeharibu vyakula vya wananchi.

Uchunguzi wa awali wa Polisi, Kamanda huyo alisema, unaonyesha kwamba nyumba nyingi ziliezuliwa kutokana na aina yake ya ujenzi na upauaji wa paa.

Alisema nyingi hazijapauliwa kitaalamu bali zimewekwa mbao na mabati juu kisha kuwekewa mawe kwa nia ya kuongeza uzito badala ya kufungwa makoa na kugongelewa misumari.

Mkoa wa Singida umekuwa ukiathiriwa mara kwa mara na upepo mkali unaombatana na mvua, wataalamu wakisema ni kutokana na jiografia yake ya kutokuwa na miti.

Miaka mitatu iliyopita, watu watano wakiwemo watoto watatu wa familia moja, walifariki wilayani Iramba na wengine wawili kujeruhiwa kwa kuangukiwa na nyumba za tembe wakati wakiwa usingizini; kutokana na mvua kubwa zilizonyesha usiku.

No comments :

Post a Comment