dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 21, 2017

MAELEKEZO YA MAISHA KATIKA QUR'AN!


*1_Usizungumze kwa ukali (3:159)*

*2_Jizuie na hasira (3:134)*

*3_Kuwa mwema kwa wengine (4:36)*

*4_Usiwe mwenye kiburi(7:13)*

*5_Samehe wanaokukosea (7:199)*

*6_Zungumza na watu kwa upole (20:44)*

*7_Shusha sauti yako (31:19)*

*8_ Usiwakejeli wengine (49:11)*

*9_Watendee wema wazazi wako (17:23)*

*10_Usiseme maneno ya kuwakosea adabu wazazi wako                 (17:23)*

*11_Usiingie chumba cha wazazi wako bila kuomba idhini              (24:58)*

*12_Andikishianeni mnapokopeshana (2:282)*

*13_Usifuate rai ya yeyote kibubusa (2:170)*

*14_Muongezee unayemdai muda wa kulipa deni kama ana hali ngumu         
       (2:280)*

*15_Usile riba (2:275)*

*16_Usijihusishe na rushwa (2:188)*

*17_Usivunje ahadi (2:177)*

*18_Tunza amana (2:283)*

*19_Usiufiche ukweli unaoujua (2:42)*

*20_Wahukumu watu kwa haki (4:58)*

*21_Simamia haki (4:135)*

*22_Mali za marehemu zigawiwe kwa warithi wao (4:7)*

*23_Wanawake pia wana haki yakurithi (4:7)*

*24_Usile Mali ya yatima (4:10)*

*25_Watunze yatima (2:220)*

*26_Msiliane Mali zenu kwa dhuluma (4:29)*

*27_Patanisheni miongoni mwa wanaogombana (49:9)*

*28_Jiepushe nakuwajengea watu Dhana mbaya (49:12)*

*29_Msipelelezane na msisengenyane (2:283)*

*30_Msipelelezane au msisengenyane (49:12)*

*31_Toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu (56:7)*

*32_Jihimizeni kuwalisha maskini (107:7)*

*33_Watafuteni wenye kuhitaji muwasaidie (2:283)*

*34_Usitumie ovyo pesa zako (17:29)*

*35_Msiharibu sadaka zenu kwa masimulizi (2:264)*

*36_Wakirimu wageni (51:26)*

*37_Waamrishe watu kutenda mema baada ya wewe mwenyewe kuyatenda            (2:44)*

*38_Msifanye uharibifu katika Ardhi (2:60)*

*39_Msiwazue watu kuingia misikitini (2:114)*

*40_Piganeni na wale wanaowapigeni tu (2:190)*

*Pendelea upatapo Msg ya Dini kama hii mtumie Mwenzio, hii ni sadaka Jariya yako na Waislam Wenzako*

No comments :

Post a Comment