dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 9, 2017

Migomba yakatwa Pemba, Waziri Aboud atembelea na kusikitishwa na ukataji wa migomba!

Ikiwa jitihada kubwa za viongozi wa dini, kisiasa na wa kijamii zimepita za kutuliza munkari wa kisiasa visiwani Pemba  bado hali katika baadhi ya maeneo visiwani humo  inaonekana si shwari.

Hii ni kutokana na tukio la usiku wa kuamkia leo  la kukatwa migomba isiyopungua  38  mali ya Bi shufaa Asaa Mwombwa  kwa kile kinachodaiwa kua ni itikadi za kisiasa.

Akikagua shamba la migomba hiyo huko Nyali Mtambwe  mara baada ya kupata taarifa hizo Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wapili wa Rais , Mohamed  Aboud   ameonyesha kukerwa na tukio hilo huku akisema kua serikali itahakikisha inawatia mbaroni wale wote watakaobainika kuhusika  na tukio hilo na sheria zitachukuliwa dhidi yao ili kukomesha hali hiyo.

Amesema kama ni uchaguzi umeshamalizika na Dk shein ndie raisi wa Zanzibar, hivyo vitendo vya kukata miti na kuhujumu haviwezi kumuondoa madarakani.Kwengineko Uwondwe Mtambwe nako miche ya miti mbalimbali isiyopungua  1100  ya wananchi wa kaya maskini zinazodhaminiwa na TASAF   imechomwa  moto usiku wa kuamkia leo na watu wasio fahamika.

Sheha wa shehia ya Mtambwe kaskazini  Suleiman Bakari Khamis mbele ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wapili wa Rais , Mohamed  Aboud  Muhammed  pia aliyetembelea eneo hilo amesema kua miti hiyo ni kwaajili ya kuotosha katika maeneo yao ili kuhifadhi mazingira lakini baadhi ya viongozi wa CUF kwa makusudi wamekua wakipita nyumba hadi nyumba  kuhamasisha watu wasishiriki katika shuhuli hizo.

Alipoulizwa na waziri huyo  juu ya wanaodhaniwa kua watendaji wa  tukio  hilo amesema kua watu hao wanawajua  hasa kwakua hawataki kuona mashirikino na mafanikio katika shuhuli hizo.

Waziri Aboud kwa upande wake amewasisitiza wananchi hao kuendelea na kazi zao hizo za kimaendeleo huku akiwa akisema kua serikali watashirikiana na mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania na kamishna wa jeshi hilo Zanzibar kuleta timu kutoka makao makuu Dar es salaam ije ifanye kazi ya kuchunguza nani wahusika wa tukio hilo na wote watakao tambuliwa hatua  za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Katika hatua nyengine waziri huyo amesema kua watafanya kura ya siri kwa wananchi wa maeneo hayo ili kueleza nani wahusika wa tukio hilo ili wapate kubainika na sheria ichukue mkondo wake.

No comments :

Post a Comment