dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 16, 2017

Deni la umeme Zanzibar kero ya Muungano!

By Salim Said Salim
Mjadala wa deni la umeme ambalo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linaidai Zanzibar umekuja juu kwa mara nyingine na kuutikisa Muungano.
Chanzo cha mtikisiko huu kilitokana na taarifa ya karibuni iliyoeleza kwamba Rais John Magufuli aliitaka Tanesco ifikapo mwisho wa mwezi huu iwakatie umeme wadaiwa wote sugu, ikiwamo Zanzibar kama hilipi deni lake la Sh121 bilion.
Lakini Zanzibar inasema kiwango hicho inachoambiwa inadaiwa na Tanesco haikitambui na kwamba ukubwa wa deni ni kama Sh67 bilioni. Nani anasema kweli na nani andanganya sielewi, lakini hiki ni kielelzo cha
hili tatizo kuwa si dogo kama inavyofikiriwa.
Agizo la Rais Magufuli limezua mjadala mkubwa Bara na Visiwani na kuzusha masuala mengi, mojawapo ni hatma ya Muungano kama huduma ya umeme visiwani itakatwa.
Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo aliporudi kutoka nje ya nchi, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alionyesha matumaini kwamba umeme
hautkatwa kutokna na kile alichokieleza kama maelewano mazuri yaliyopo kati ya pande hizi mbili za Muungano.
Lakini akasema ikiwamo hilo likitokea, Wazanzibari watafanya kile kinachoitwa lisilo budi hutendwa. Nacho ni kutegemea kibatari kupata mwanga.
Kurejea kutumia kibatari, kandili, mshumaa, karabai na njia nyengine za asili kupata mwangaza kwenye kiza katika nusu karne iliyopita ni kuendeleza kilichoonekana mara nyingi Visiwani katika miaka ya karibuni.
Kwa wanaojua mashamshamu ya mashabiki wa burdani wanapovutiwa na wimbo ni ile kauli ya “Once more”, yaani rudia tena.
Kukatwa kwa huduma ya umeme si tu kutazusha mtafaruku katika majumba, lakini kutaathiri sana shughuli nyingi katika ofsi za Serikali na Sekta Binafsi, shule, hospitali, viwanda, kilimo na utalii.
Hili deni la Tanesco ambalo limekuwa si kama hilo tunalosikia siku hizi likiitwa jipu linalohitaji kutumbuliwa, bali ni suala zito lililozungukwa na mambo yanayozungumzwa chini kwa chini na mengine kwa uwazi.
Ukiliangalia kwa undani utakuta hili suala la umeme limeingia katika orodha ya mambo yanayoguswa kama kero za Muungano unaotimiza miaka 43 tangu kuanzishwa.
Kwanini kero
Labda nigusie kwa muhtasari inakuwaje hata malipo ya umeme yawe kero za Muungano? Huu umeme kutoka Bara ambao unapelekwa kisiwa cha Unguja na waya uliotandazwa baharini ulilipiwa gharama zake zote za vifaa na vingine na Serikali ya Zanzibar.
Mbali ya hilo, palipotokea matengenezo makubwa, kama kutandazwa waya mwingine baada ya ule wa awali uliotumika kwa miongo mitatu kutoweza tena kufanya kazi kutokana na uchakavu, mwaka 2010 Zanzibar ndiyo iliyolipa gharama zote za kazi hio.
Sasa kwa kuwa ada za malipo ya umme za Tanesco utilia maananani gharama zinazotumika kumpelekea mteja huduma na kufanya matengezo, Zanzibar imekuwa ikilalamika kwamba haipaswi kutozwa ada kama za wateja waliopo Bara kwa sababu ililipia kufikisha huduma hiyo visiwani.
Hili limekuwa likilalamikiwa sana na ipo vuta nikuvute ambayo huwa haizungumzwi kwa uwazi ili Watanzania wa bara na Visiwani kuielewa kwa undani.
Lakini yapo maeneno mengine ambayo Zanzibar imekuwa ikilalamika kuwa haikutendewa haki na Serikali ya Muungano na inapodai kile inachokiona ni fedha zake halali hailipwi.
Orodha ni ndefu na miongoni mwa mambo ambayo hugusiwa ni mgao wa fedha za kigeni za Zanzibar baada ya kuvunjika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na kila nchi kuwa na sarafu yake.
Fedha hizi, kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mara kwa mara naviongozi wa Serikali ya Zanzibar na wataalamu wa uchumi zilitumika kama mtaji wa kunzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), lakini Zanzibar haipati kiwango kinachostahiki cha faida inayotengenezwa na BoT.
Undani wa suala hili haupo wazi kwa vile hakuna upande wa Muungano unaolitolea maelezo ya wazi. Kimya kimezusha uvumi wa kila aina.
Wazanzibari wamesikika wakilalamika kuwa vipo vifaa vilivyonunuliwa na Zanzibar kwa fedha nyingi za kigeni, kama ndege na meli, ambazo huonekana zikipaa angani wakati wa sherehe na meli moja inayofika Zanzibar mara kwa mra kutoka Dar es Salaam zimechukuliwa na Serikali ya Muungano na haikulipwa hata shilngi.
Katikahali hii ndiyo unasikia malalamiko kwa nini Zanzibar inapodaiwa kama malipo ya huduma ya umeme panasikika kauli za kusimbuliana na unyanyasaji wakati na Zanzibar nayo inayo madai yake kwa Serikali ya
Muungano, lakini yamefumbiwa macho.
Kwa hakika kuyakalia matatizo haya yanayoitwa kero za Muungano na kutotafuta njia muafaka ya kudumu ya kuyatatua kutazalisha chuki na kutoaminiana kwa pande hizi mbili na gharama zake kuwa kubwa kwa mustakbali wa Mungano.
Hizi zinazoitwa kero za Muungano zimeundiwa kamati ndogo, kamati kubwa, kamati maalum, tume na vikao vingi kutafuta marekebisho yatayoleta muafaka na kuacha kulaumiana na kutishana.
Lilio wazi ni kwamba kila tukikawia kupata ufumubuzi wa uhakika na badala yake kutoka na taarifa za “tupo mbioni” na maelezo yanayofanana kila siku, tofauti ikiwa ni tarehe ya hiyo taarifa, msuguano katika Muungano utaongezeka.
Wapo waliotegemea mchakato wakupata katiba mpya ngesaidia angalau upunguza na kuhakikisha hizo kero za Muungano haziongezeki.
Lakini mchakato wa Katiba ambao ulikuwa na mvutano mkubwa na kugharimu mabilioni ya shilingi umewekwa pembe za chaki na hakuna anayejua kitachofuata.
Kwa kawaida ndugu, kama Watanzania wa Bara na Visiwnai tunavyojiita baada ya kuungana mwaka 1964, huwa hawatarajiwi kuhesabiana ‘mie nimekupa hiki na wewe umenipa hiki’.
Baya zaidi ni pale upande moja unaposhikilia lake na kutoa kauli ambazo huutia unyonge upande mwingine wa Muungano kama hili tishio la kukata umeme.
Nii kitatokea katika sakata hii ya umeme ni tabu kutabiri kwa vile ni kiza kitupu na hakuna mwanga unaotoa ishara ya nini kitafayika kumaliza hii vuta nikuvute ya deni la Tanesco.
/Mwananchi.

No comments :

Post a Comment