dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, March 18, 2017

Muuguzi aburuzwa kortini kwa kugushi vyeti!

Moshi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewaburuza kortini watu wanne akiwamo muuguzi mwandamizi wa Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi, anayedaiwa kugushi  cheti cha shahada ya kwanza.

Muuguzi huyo, Hawa Nyanga alipandishwa kizimbani jana mjini Moshi, mbele ya Hakimu Mkazi Anthony Ngowi akidaiwa kughushi cheti kinachoonyesha kuwa amehitimu shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Texas Women cha nchini Marekani.

Waendesha mashitaka wa Takukuru wakiongozwa na Barry Galinoma akisaidiana na Caroline Lugenge na Furahini Kibanga, walidai kuwa Oktoba 17, mwaka 2011, Hawa alikiwasilisha cheti hicho na matokeo (Academic transcript) kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS).
Kwa mujibu wa waendesha mashitaka hao wa Takukuru, muuguzi huyo aliwasilisha cheti hicho kinachodaiwa kuwa ni cha kughushi kwa RAS huku akijua si cha kweli, kitendo ambacho ni kinyume cha kifungu 342 na 337 cha kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Hata hivyo, mshitakiwa alikana mashtaka hayo na aliachiwa kwa dhamana ya maneno ya Sh3 milioni hadi Aprili 19 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa kwa mara nyingine mahakamani hapo.

Katika kesi nyingine, Takukuru imewafikisha mahakamani viongozi wa zamani watatu wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos) cha Manispaa ya Moshi, wakituhumiwa kukiibia chama hicho Sh11.1 milioni.

Washtakiwa hao waliofikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anthony Ngowi ni Peter Ndelianarua aliyekuwa meneja, Gerald Msacky aliyekuwa mhasibu na Rehema Mlay aliyekuwa mtunza fedha.

Waendesha mashtaka wa Takukuru, Galinoma, Lugenge na Kibanga walidai kuwa kati ya Januari 1, 2013 na Desemba 31 mwaka huo huo, washtakiwa kwa pamoja waliiba kiasi hicho cha fedha mali ya mwajiri wao.

Washitakiwa kwa pamoja walikana mashtaka na wawili waliachiwa huru kwa dhamana ya maneno ya Sh3 milioni hadi Machi 31 kesi itakapotajwa tena,  huku mwenzao Peter ambaye ni mshtakiwa wa kwanza  akishindwa kutimiza masharti ya dhamana na alijikuta akipelekwa mahabusu.Takukuru yamburuza kortini muuguzi kwa kughushi cheti.

No comments :

Post a Comment