dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 26, 2017

Makamu wa Rais Samia Suluhu: Kero za muungano kutatuliwa!


Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, amewahimiza wananchi kudumisha na kuuenzi Muungano wa Taganyika na Zanzibar na kuwahakikishia wananchi wa pande hizo mbili kuwa kero chache za Muungano zilizobakia zitamalizwa kwa mazungumzo

Mh. Samia ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari katika kuelekea katika Kilele cha Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo sherehe za kitaifa mwaka huu kwa mara ya Kwanza zitafanyika Mjini Dodoma.

Amesisitiza kuwa, tangu Muungano huo uasisiwe umekuwa na manufaa makubwa kwa pande zote mbili kwani jamii zimefahamiana na kushirikiano vizuri katika shughuli za kiuchumi na za kimaendeleo hasa uimarishaji wa ulinzi na usalama kwa wananchi wa pande mbili.

Aidha, amesema, hatua zinazochukuliwa za kutatua kero za Muungano kwa haraka ni jambo jema na la msingi kwani linalenga kuhakikisha Muungano ambao umefikisha miaka 53 sasa unakuwa ni Muungano wa mfano wa kuigwa Duniani.

Kuhusu elimu ya Muungano wa vijana, Makamu wa Rais amesema upo umuhimu mkubwa kwa taasisi za kiserikali za pande mbili kuweka mikakati mizuri ya kuelimisha vijana wa sasa kujua umuhimu wa Muungano ili waweze kuuelewa na kuudumisha.

Mh. Samia amesema kwa sasa vijana wengi wanafuatilia sana mitandao ya kijamii hivyo ni muhimu kwa taasisi za kiserikali zinazoshughulia Muungano kuweka utaratibu wa kupeleka ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano kwa jamii hasa vijana kwa ajili ya kuwaelimisha faida za Muungano.
Makamu wa Rais pia amehimiza makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi wastaafu nchini waendelee na jitihada zao katika kuelimisha umma ili kuuelewa vizuri Muungano kwa ajili ya faida ya jamii nzima na ya Taifa kwa ujumla.

1 comment :

  1. Kweli Bi Samia umenena ukweli kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa lakini hukusema dhidi ya nani? tunavyo fahamu huo ulinzi na usalama ni wa kumgandamiza Mzenji asiinue sauti ya kuomba usawa katika haki zake za kikatiba ambazo chama tawala toka bara kwa miaka 53 mmekuwa watawala weusi dhidi ya weusi..ndio maana hata bendera ya Tanzania imepeperushwa jijini London katika kanisa moja maarufu ikiwa ni kuwaunga mkono wapokaji wa kibara!

    Mimi sioni cha kujivunia na huo muungano zaidi ya kunyanyaswa na magaidi toka bara kila kukicha...nini cha kujivunia wazenji? Muungano wa kulazimishwa kwa mtutu wa bunduki? sidhani kuwa kwa mwenye akili timamu ataunga mkono huo muungano...hayo matatizo machache anayo yataja Bi Samia sio machache bali ni huo udikteta wa CCM wa miaka 53 sio mdogo! Mentality za CCM lazima zibadilike kuwa Mzenji ni partners sio adui na wakubali kushindwa katika chaguzi za kuchagua kiongozi wa kuwaongoza sio lazima CCM ndio itawale milele, kwani hio nchi au hizo nchi ni mali ya wana-CCM pekee yao? the party has to inclusive..

    ReplyDelete