Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZSSF

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Tuesday, September 26, 2017

Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB Yatoa Elimu ya Walipa Kodi Kwa Wafanyabiasha Kisiwani Pemba leo!


Meneja Sera, Utafiti, na Mipango kutoka ZRB Zanzibar Ahmed Saadat, akifafanua jambo kwenye semina kwa wafanyabishara, juu ya kuelezwa mabadiliko ya sheria mbali mbali za kodi mafunzo hayo, yalifanyika mjini Chakechake hivi karibuni
Afisa Mwandamizi wa ZRB elimu kwa walipa kodi kutoka ZRB Zanzibara, Shaaban Yahya Ramadhan, akiwaeleza wafanyabiashara juu ya muamala wa kupitia simu ya mkononi kulipa kodi zao, kwenye semina iliofanyika hivi karibuni mjini Chakechake, kisiwani Pemba

Afisa Mwandamizi wa ZRB elimu kwa walipa kodi kutoka ZRB Zanzibara, Shaaban Yahya Ramadhan, akiwaeleza wafanyabiashara juu ya muamala wa kupitia simu ya mkononi kulipa kodi zao, kwenye semina iliofanyika hivi karibuni mjini Chakechake, kisiwani Pemba.

US says it's not pushing for regime change in North Korea!


KUTOKA MAGAZETI YA TANZANIA YA LEO TAREHE 26 SEPTEMBER, 2017!
MASAUNI AFANYA ZIARA WILAYANI RUFIJI, ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI!


Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya kikazi ikiwa lengo ni kukagua masuala ya Ulinzi na Usalama na kusikiliza maoni na kero za wananchi.Mkutano huo ulifanyika katika Viwanja vya Ikwiriri, wilayani Rufiji, mkoani Pwani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa, akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), ikiwa lengo ni kukagua masuala ya Ulinzi na Usalama na kusikiliza maoni na kero za wananchi.Mkutano huo ulifanyika katika Viwanja vya Ikwiriri, wilayani Rufiji,mkoani Pwani. 
Wananchi wakifurahia jambo kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), ikiwa lengo ni kukagua masuala ya Ulinzi na Usalama na kusikiliza maoni na kero za wananchi.Mkutano huo ulifanyika katika Viwanja vya Ikwiriri, wilayani Rufiji, mkoani Pwani.

Myweather anunua jumba la bilioni 56!

 KWA watu wengi, kumiliki majumba Las Vegas na Miami ingetosha kuwafanya waone wameshamaliza kazi, lakini Floyd Mayweather yupo tofauti na wengi.

Bondia huyo Mmarekani ambaye hajawahi kupigwa katika pambano lolote kati ya mapambano yake 50 aliyocheza, anaendelea ku­furahia maisha ya kustaafu baada ya kumchapa Muiri­shi, Conor McGregor jijini Las Vegas.

Baada ya kumchapa McGregor katika raundi ya 10, inadaiwa Mayweather aliweka kibindoni zaidi ya pauni milioni 250 (Sh bil­ioni 752).

Bondia huyo ambaye amekuwa hajivungi ka­tika matumizi ya fedha na kufurahia jasho lake, amemwaga kitita cha pau­ni milioni 18.9 (zaidi ya Sh bilioni 56) kununua jumba kubwa la kifahari, katika eneo la watu wazito la Beverly Hills.

DAKTARI AANIKA KUHUSU VYUMA VINNE KWENYE MOYO WA MANJI!

Image result for Manji na Wakili wake, Hajra Mungula.
Manji na Wakili wake, Hajra Mungula.
DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Aga Khan, Mustapha Bapumia (62) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anashangaa mtu mwenye umri mdogo kama Yusufali Manji (41)kuwa na vyuma vinne kwenye moyo.

Alieleza kuwa na vyuma vinne kwenye moyo ni hatari na kwamba anatembea katika kamba nyembamba. “Kitaaluma huyu ni lazima ajiangalie sana yupo katika hatari anaweza kupoteza maisha muda wowote.”

Dk Bapumia ambaye ni shahidi wa tatu wa upande wa utetezi alimeeleza hayo leo Jumatatu mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akitoa ushahidi katika kesi inayomkabili Manji ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroine.

Polepole azungumzia madiwani wa Chadema waliohamia CCM!

Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey
Dar es Salaam. Siku chache baada ya diwani mwingine wa Chadema mkoani Arusha kujiunga na CCM, katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole amesema tukio hilo halikuwa limeandaliwa.

Diwani huyo wa Kimandolu (Chadema), Mchungaji Rayson Ngowi alitangaza kuihama Chadema dakika chache baada ya Rais John Magufuli kutoa fursa kwa wanachama wa vyama tofgauti kutangaza kujiunga na vyama vingine.

Tukio hilo lilifanyika wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa maofisa 422 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.