dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 23, 2017

KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR, AFANYA ZIARA OFISI YA UHAMIAJI MKOA WA KUSINI UNGUJA!

 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu akielezea jinsi Idara ya Uhamiaji inavyopiga hatua katika kutatua changamoto ya Makaazi ya Askari wake katika Wilaya zote Unguja na Pemba. Aliayasema hayo wakati akikagua nyumba za Watumishi wa Uhamiaji iliyopo Makunduchi, Wilaya ya Kusini wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika tarehe 21 - 22 Novemba, 2017.
 Maafisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, wakiambatana na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (katikati) alipofanya ziara ya kikazi Wilaya ya Kati na Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 21 - 22 Novemba, 2017, wakipokea taarifa kuhusu mkakati wa kuboresha Ofisi na Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, Mkoani humo. Ziara hiyo ililenga kukagua Miradi ya Idara pamoja na Viwanja vilivyopo Mkoani wa Kusini Unguja. Ikiwa ni hatua muhimu katika kutanua wigo wa utoaji huduma mbali mbali za Uhamiaji kwa Wilaya zote za Unguja na Pemba. Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi za Serikali kuwafikishia wananchi wake huduma katika maeneo wanayoishi.
 Afisa Uhamiaji Wilaya ya Kusini Mkaguzi Msaidizi  wa Uhamiaji, Kheri Shabani akisalimiana na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wakati alipowasili kwenye Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo,   tarehe 21 - 22 Novemba, 2017.
 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, akitia saini kitabu cha wageni, mara tu alipowasili Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni mwendelezo wa  ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 22 Novemba, 2017.  Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Mkemimi Mohamed Mhina.
 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, Akijibu hoja mbali mbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 21 - 22 Novemba, 2017.  Kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdullah Mbarouk Ramsa.
 Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Khamis Ali Juma akitoa maoni juu ya changamoto wanazokabiliana nazo katika eneo la uendeshaji wa mashtaka ya Kiuhamiaji, wakati wa kikao cha pamoja cha Wafanyakazi wa Mkoa wa Kusini Unguja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 21 - 22 Novemba, 2017.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kati kati), akifatilia kwa makini majadiliano katika kikao cha pamoja na watumishi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 21 - 22 Novemba, 2017. Kulia ni Afisa Uhamiaji Mkoa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Mkemimi Mohamed Mhina na Kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdullah Mbarouk Ramsa.

No comments :

Post a Comment